Madereva wa daladala Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya kuacha mara Moja tabia ya kusimama ghafla barabarani pindi wanapoona Kuna abiria anahitaji usafiri.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewataka madereva wote wa daladala kuacha tabia hiyo badala yake wasimame kwa kuzingatia usalama Kwa watumiaji wengine wa barabara ili kuepusha ajali zisizo za lazima.Lakini pia Sajenti Ndimila amewataka Abiria kuwa na tabia ya kutoa taarifa Kwa mamlaka husika pindi waonapo vitendo hatarishi vya namna hiyo vikitendeka barabarani.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment