
Farida Mangube, Morogoro
Gidioni Mbwambo(34)mkazi wa Manispaa ya Morogoro amekutwa amejiua kwa kujikata Koromeo kwa kutumia kitu chenye makali kwenye nyumba ya kulala wageni na inadaiwa alikuwa amelewa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama tukio hilo lilitokea Januari 27,2026 Majira ya asubuhi katika nyumba ya kulala wageni ya Kisanga iliyopo mtaa wa nguzo Kata ya Mazimbu.
Amesema marehemu alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba namba 106 Januari 26,2026.
Kamanda Mkama amesema iligundulika baada ya michilizi ya damu na maji ikitokeza nje ya chumba alichopanga marehemu.
“Baada ya kuvunjwa mlango uliokuwa umefungwa kwa ajili ya uchunguzi ilibainika alikufa na alikuwa na jereha la kujitaka Koromeo eneo la shingo kwa kutumia kitu chenye makali,”alisema.
Aidha amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu amejiua kwa kutumia kifaa hicho na kwamba alikuwa katika hali ya ulevi.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limetoa wito kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwa makini na kufuata taratibu zote za kutambua wageni,ili inapotokea changamoto kama hiyo iwe laisi kutambuliwa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment