" Ali Kamwe Awachokoza Simba Baada ya Kufungwa

Ali Kamwe Awachokoza Simba Baada ya Kufungwa

 

Msemaji wa klabu ya Yanga Ali Kamwe hajataka kabisa hili limpite baada ya klabu ya Simba kupoteza mchezo wa tatu katika hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika. Ali Kamwe ni miongoni katika waliofurahia Zaidi Simba kupoteza mchezo huo wa siku ya Jana.

Kupitia Instagram Yake Ali Kamwe alindika ” wamegawa Tena kwenye baridi Kali” akisindikiza na emoji nyingi za kicheko Kikali. Kauli hiyo imefuatana na kauli ya msmaji wa Simba ambaye aliwahi kusema katika kila kundi yupo mmoja ambaye atakua akigawa utamu Kwa Wenzake. Na sasa imerudi kwa Simba.

Yanga Kubadilishiwa Ratiba

Kwa upande mwingine Klabu ya Yanga SC imebadilishiwa rasmi ratiba yake ya michezo mara baada ya kurejea jijini Dar es Salaam ikitokea nchini Misri, ambako ilikuwa na majukumu ya kimataifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mabadiliko hayo yamelenga kuipa timu nafasi ya kujiandaa vizuri kimwili na kiakili kabla ya kuendelea na ratiba ngumu ya mashindano ya ndani na nje ya nchi.Kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara sasa wataanza kwa kucheza mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji FC, utakaopigwa tarehe 27 Januari katika Uwanja wa KMC Complex, kuanzia saa 1:00 usiku. Awali, Yanga ilikuwa imepangiwa kukutana na Azam FC, lakini mchezo huo umeondolewa kwa muda na nafasi yake kuchukuliwa na huu wa Dodoma Jiji.

Uamuzi wa kuipa Yanga mchezo wa ligi kwanza unaelezwa kuwa ni sehemu ya mpango wa kusaidia kikosi kurejea kwenye mzunguko wa mashindano ya ndani baada ya safari ndefu na mechi zenye presha kubwa barani Afrika. Benchi la ufundi linaamini kuwa mchezo huo wa Dodoma Jiji utakuwa muhimu katika kurejesha hali ya ushindani kwa wachezaji, pamoja na kufanya marekebisho ya kiufundi kabla ya kibarua kigumu kijacho.

Baada ya kumaliza mchezo huo wa Ligi Kuu, Yanga SC inatarajiwa kusafiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi maalum ya maandalizi kuelekea mchezo mkubwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, utakaochezwa tarehe 31 Januari. Mechi hiyo inatajwa kuwa miongoni mwa michezo muhimu zaidi kwa Yanga katika hatua ya makundi, kutokana na uzito wa mpinzani na umuhimu wa pointi tatu.

Kwa mashabiki wa Yanga, mabadiliko haya ya ratiba yanachukuliwa kama fursa ya kuona kikosi kikirudi katika uwanja wa nyumbani kabla ya kuingia tena kwenye anga za kimataifa. Aidha, ni nafasi kwa kocha Pedro Gonçalves kupima kiwango cha wachezaji wake, kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza Misri, na kuweka mkakati madhubuti wa kuivaa Al Ahly.

  

Post a Comment

Previous Post Next Post