Na Ngonise Kahise, Misalaba Media-Dar Es Salaam Serikali imesema Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga unatarajiwa kufungua ajira zisizopungua 12,000 na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na nchi jirani za Afrika Mashariki.Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 5, 2025, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratias Ndejembi, alisema mradi huo ni wa kimkakati na una mchango mkubwa katika kuimarisha mapato ya serikali, kukuza biashara na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.“Mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati itakayochangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi,” alisema Mhe. Ndejembi.Amesema mradi huo unatarajiwa kugharimu takribani dola za Marekani bilioni 79 na kukamilika ifikapo Julai mwaka 2026, huku ukiwa chanzo kikubwa cha ajira wakati wa kipindi cha ujenzi.“Katika utekelezaji wa mradi huu, zaidi ya ajira 12,000 zitafunguliwa, na Watanzania watanufaika kwa kiwango kikubwa kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,” aliongeza.Mhe. Ndejembi ameeleza kuwa baada ya kukamilika, mradi huo utaipatia Tanzania mapato makubwa kupitia shughuli za usafirishaji wa mafuta ghafi, hatua itakayoongeza mapato ya serikali na kuimarisha uchumi wa taifa.“Tanzania inatarajiwa kupokea mapato yanayokadiriwa kufikia zaidi ya tani 246,000 kutokana na shughuli za usafirishaji wa mafuta ghafi kupitia bomba hili,” alisema.Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Dkt. Ruth Nankabirwa, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi na ushirikiano mkubwa ulioiwezesha miradi ya kimkakati kutekelezwa kwa mafanikio.“Ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Uganda umewezesha mradi huu kufikia hatua kubwa, na tuna imani utafungua fursa nyingi za uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi kwa nchi zetu,” alisema Dkt. Nankabirwa.Ameongeza kuwa mradi huo utaimarisha mahusiano ya kiuchumi, kuboresha miundombinu na kukuza biashara kati ya Tanzania, Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki.Mradi wa bomba la mafuta ghafi una urefu wa kilomita 1,443, ambapo kilomita 296 zipo nchini Uganda na kilomita 1,147 zipo nchini Tanzania. Bomba hilo litakuwa na vituo vinne vya kusukuma mafuta nchini Uganda na vituo viwili nchini Tanzania.Serikali imesisitiza kuwa utekelezaji wa mradi huo unazingatia kikamilifu masuala ya mazingira, usalama na ustawi wa wananchi ili kuhakikisha maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment