
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 17,2026 jijini Dodoma
Na.Alex Sonna-DODOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kukutana na Mabalozi wa Tanzania Januari 15, 2026 katika kikao cha ufunguzi wa mwaka, hatua iliyotajwa kuongeza hadhi ya nchi kimataifa na kuonyesha mwelekeo chanya wa diplomasia ya taifa.
Pongezi hizo zimetolewa leo Januari 17, 2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
"Mkutano huo kati ya Rais Samia na mabalozi umeonyesha dhamira ya Serikali kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa huku ukaleta taswira nzuri ya Tanzania katika medani za diplomasia na uchumi."amesema Kihongosi
Aidha, Kihongosi ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi, ambapo makusanyo yamefikia shilingi trilioni 3.1 na mwezi Desemba pekee kuvuka zaidi ya shilingi trilioni 4, akisema hatua hiyo inaonyesha ufanisi mkubwa katika usimamizi wa mapato ya Serikali.
Katika masuala ya kijamii, Kihongosi amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya uzinduzi wa Bima ya Afya kwa Wote, sambamba na kuchukua hatua za kuondoa utaratibu wa kuzuiliwa kwa maiti pale wagonjwa wanaposhindwa kulipia gharama za matibabu.
Ameongeza kuwa Serikali imetekeleza ahadi ya ajira kwa kutoa zaidi ya ajira 12,000 katika sekta mbalimbali, huku mpango wa kutoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi ukiendelea kutekelezwa.
Katika hatua nyingine Kihongosi,ametoa onyo vikali dhidi ya kauli na mienendo inayopotosha ukweli, kuchafua historia ya taifa na kuhujumu amani kwa maslahi binafsi, kikisisitiza kuwa hakitaruhusu siasa za jazba, chuki na migawanyiko.
Kihongosi amesema CCM ni chama kinachojengwa juu ya misingi ya maridhiano umoja na kuheshimiana hivyo hakitovumilia juhudi zozote za kupotosha ukweli au kueneza chuki zisizo na tija kwa Taifa.
Amesema CCM inamheshimu Waziri Mkuu na Jaji Mkuu Mstaafu Joseph Warioba kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa lakini ikamtaka kuendelea kufurahia maisha ya kustaafu kwa utulivu bila kutoa malalamiko.
"Ni jambo la kawaida kwa viongozi waliotumikia Taifa kuheshimiwa lakini wastaafu wanapaswa kutoa nafasi kwa viongozi waliopo kuendelea na majukumu yao Kihongosi, "amesema
Ameongeza kuwa "Licha ya Jaji Warioba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan bado alionekana mitandaoni akitoa kauli zenye malalamiko hali aliyoitaja kuwa haina tija kwa maendeleo ya Taifa, ".
Kuhusu ziara ya kitaifa Kihongosi amesema kuanzia Januari 18 2026 ataanza ziara ya kichama itakayohusisha mikoa yote ya Tanzania kuanzia mkoani Singida Ziara hiyo inalenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi kuimarisha chama na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Rais Samia
" Ziara hii ni jukwaa la wananchi kama kuna anayehisi kuonewa au kunyanyaswa tunawakaribisha waje ili tusikilize na kutatua changamoto zao, "Kihongosi
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment