" GENERALI MUSEVENI APITA KWA KISHINDO MBIO ZA URAIS

GENERALI MUSEVENI APITA KWA KISHINDO MBIO ZA URAIS

Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media- Uganda.

‎Tume ya Uchaguzi imemtangaza  Mwanasiasa  Mkongwe na Jeneraki wa zamani  wa jeshi la Uganda.Yoweri Kaguta Museveni, mwenye umri wa Miaka 81, kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Uganda uliofanyika Januari 15, 2026, akipata Asilimia 71.6 ya jumla ya kura halali zilizopigwa, na kuendeleza utawala wake zaidi ya miongo minne na kuwashinda wapinzani wake Kwa kishindo kikubwa cha  kiasi cha kura zilizopigwa na Wananchi wa Uganda na kumpa ushindi wa kishindo.

‎Hata hivyo, chama cha Bobi Wine  kimehoji uhalali wa matokeo hayo, kikidai kuwa kiongozi huyo wa upinzani alichukuliwa kwa nguvu kutoka nyumbani kwake jijini Kampala,Madai ambayo  yamepingwa na mamlaka  ya nchini hapa  msemaji wa polisi alisema hawana taarifa hiyo.

‎Aidha mamlaka ya mawasiliano nchini hapa "UCCA' ilizima mtandao wa internet Kwa lengo la kudhibiti udanganyifu na taarifa potofu wakati wa uchaguzi.


  


Post a Comment

Previous Post Next Post