Na Lydia Lugakila -Misalaba Media
Kyerwa
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Bi. Zaitun Msofe, amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kuendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi kwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuzingatia maslahi ya jamii hatua itakayosaidia kudumisha amani na kuondoa migogoro isiyo ya lazima katika jamii.
Bi. Msofe ametoa kauli hiyo Januari 30, 2026, wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukijadili taarifa ya utekelezaji wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa.
Amesisitiza kuwa maamuzi ya madiwani yana mchango mkubwa katika kuimarisha mshikamano.
Msofe Amewahimiza pia madiwani hao kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa Serikali wa Bima ya Afya kwa Wote, ambapo kila kaya huchangia kiasi cha shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) kwa mwaka ili kupata huduma za matibabu bila vikwazo.
Pamoja na hayo, DC Msofe amesisitiza madiwani pamoja na wataalam wa elimu wa halmashauri hiyo kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mpango wa kisayansi wa kujenga umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa darasa la kwanza.
Mpango huo ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo amesema kuwa msingi wa elimu bora huanza katika ngazi za awali, hivyo ni muhimu kwa idara ya elimu ya awali na msingi kuhakikisha mpango wa KKK unatekelezwa ipasavyo ili kuwajengea wanafunzi uwezo imara wa kusoma, kuandika na kuhesabu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment