Na Lydia Lugakila- Misalaba MediaMbeyaJumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini leo imefanya matembezi ya amani ikiwa ni sehemu ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 49 tangu kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi, kilichoasisiwa Februari 5, 1977.Akizungumza mara baada ya matembezi hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Emmanuel Mwalupindi, amewataka wanachama wa chama hicho kuondoa hofu na uoga katika kukitumikia chama chao. Amesisitiza kuwa CCM ni chama chenye misingi imara, historia kubwa na mchango mkubwa katika kulihudumia Taifa tangu kuasisiwa kwake.Kwa upande wake, Katibu wa Shirikisho la Walimu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Daud Siame, ametumia fursa hiyo kuhimiza amani, mshikamano na umoja miongoni mwa wanachama wa chama hicho. Amesema kuwa mshikamano ni nguzo muhimu ya mafanikio ya chama na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.Baadhi ya wanachama walioshiriki katika matembezi hayo wameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii inayotekelezwa na CCM, ikiwemo katika sekta za elimu, afya na miundombinu. Wamesisitiza kuwa chama hicho kimeendelea kugusa maisha ya wananchi na kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.Maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi yanaendelea kufanyika nchi nzima kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na kisiasa, huku wanachama wakisisitiza umoja, amani na mshikamano kama msingi muhimu wa kuendeleza maendeleo ya Taifa.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment