" DK. MWIGULU: KUHARIBU MIUNDOMBINU NI KUJIUMIZA MWENYEWE, TUACHANE NA HUJUMA ZA KIUCHUMI

DK. MWIGULU: KUHARIBU MIUNDOMBINU NI KUJIUMIZA MWENYEWE, TUACHANE NA HUJUMA ZA KIUCHUMI

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amewatahadharisha Watanzania kuacha kutumiwa na watu wenye nia ovu kuhujumu uchumi wa nchi kwa kuharibu miundombinu, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni "kupiga ngumi kwenye ukuta na kuumiza mikono yako mwenyewe."

Akirejea matukio ya vurugu yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dk. Mwigulu amebainisha kuwa uharibifu wa zahanati, barabara na mifumo ya mawasiliano hauikomoi Serikali, bali unamuumiza mwananchi wa kawaida ambaye kodi yake ndiyo iliyojenga miradi hiyo.

Hujuma za Kiuchumi Dk. Mwigulu amefafanua kuwa vurugu hizo hazikuwa maandamano ya kidemokrasia, bali ni mbinu ya mabeberu wanaotaka kuifanya Tanzania ishindwe kuzalisha ili wao waje kuchota rasilimali kama gesi asilia ya Lindi, makaa ya mawe na madini wakati Watanzania wakimwagiana damu.

"Wanaotaka kutuvuruga wanajua kuwa tukiingia kwenye giza la vurugu, hatutakuwa na muda wa kuzalisha. Matokeo yake tutaanza kuuziwa silaha na bidhaa kwa bei wanayotaka wao huku wakijifanya wanatupa misaada," alisema Dk. Mwigulu.

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amenukuliwa akisema kuwa mafanikio ya Tanzania yanawanyima usingizi wale wanaotaka kuiona Afrika ikiendelea kuwa maskini. Amesema mabeberu hawafurahii kuona Tanzania inajitegemea kwa fedha zake yenyewe kujenga miundombinu ya kisasa.

"Tanzania haitaendeshwa kwa rimoti (remote control). Miundombinu tuliyonayo si mali ya Serikali, bali ni mali ya kila Mtanzania. Hata unaponunua shati la mtoto mchanga, unachangia ujenzi wa barabara na zahanati hizi," alisisitiza Dk. Mwigulu.

Post a Comment

Previous Post Next Post