EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD: SAFARI YA UBORA WA KIMATAIFA KUTOKA SHINYANGA HADI MEZANI KWA MTANZANIA
Katika kipindi ambacho Watanzania wamekuwa wakihitaji vinywaji vyenye ubora wa hali ya juu, ladha halisi na bei rafiki, Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd imejitokeza kama jibu sahihi la mahitaji hayo.
Kampuni hii ilianzishwa rasmi mwezi Oktoba 2017, ikiwa na makao yake makuu katika Manispaa ya Shinyanga, Tanzania, ikiwa na dhamira ya dhati ya kubadili taswira ya sekta ya vinywaji nchini.
Tangu kuanzishwa kwake, East African Spirits (T) Ltd imejikita katika kuzalisha vinywaji vyenye hadhi ya kimataifa, vinavyokidhi viwango vya ubora huku vikizingatia mazingira, afya ya mtumiaji na uwezo wa soko la ndani huku lengo kuu likiwa ni kumpatia Mtanzania bidhaa bora ambazo awali zilionekana kuwa ndoto au zilihitaji gharama kubwa kuzipata.
MWELEKEO WA KIMKAKATI: BIA NA POMBE KALI
Katika safari yake ya mafanikio, kampuni ilianza kwa kuwekeza katika sekta mbili muhimu na zenye ushindani mkubwa sokoni, ambazo ni pombe kali (spirits) na bia. Hatua hii ililenga kuwahudumia wananchi wa rika na matabaka mbalimbali kwa kuwapatia chaguo sahihi la vinywaji bora, vyenye ladha tulivu na vinavyotengenezwa kwa viwango vinavyotambulika kimataifa.
Kupitia mwelekeo huu, East African Spirits (T) Ltd imejidhihirisha kama chaguo sahihi kwa Watanzania wanaotafuta vinywaji vya hadhi, kwa bei rafiki na ubora unaoaminika.
MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA POMBE KALI (SPIRITS)
Mwaka 2017, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maono yake, kampuni ilijenga kiwanda cha kisasa cha kuzalisha pombe kali, chenye mitambo ya teknolojia ya juu inayozingatia usalama, ubora na afya ya mtumiaji.
Kupitia kiwanda hiki, kampuni imefanikiwa kuzalisha bidhaa zenye ushindani mkubwa sokoni, zikiwemo:
- Hanson’s Choice Brandy
- Diamond Rock Gin
Bidhaa hizi zimepokelewa kwa mwitikio mkubwa kutoka kwa watumiaji, wakisifia ladha laini, harufu nzuri na upekee wake, sambamba na kutokuwepo kwa athari kali za “hangover” endapo zitumike kwa kuzingatia kanuni za unywaji wa kistaarabu.
MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA BIA
Mwaka 2023, East African Spirits (T) Ltd ilipiga hatua nyingine kubwa kwa kuzindua kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bia kilichopo Shinyanga. Kiwanda hiki kimeifanya kampuni kuingia rasmi katika soko la bia kwa nguvu na ushindani mkubwa.
Kupitia kiwanda hicho, kampuni imefanikiwa kuzalisha bia tatu bora ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa sokoni:
1. Goldberg Malt Lager – 4.4% Alcohol
Beer of Our Own Class
Bia ya hadhi kwa mtu anayejitambua, mwenye kuthamini ubora, ladha tulivu na daraja la kipekee.2. Hanson’s Lite Lager – 4.0% Alcohol
The New Lite
Chaguo bora kwa wanaopenda bia nyepesi, yenye radha safi na inayofaa kwa matumizi ya kawaida bila uzito mkubwa wa kilevi.3. Basembi Extra Lager – 5.8% Alcohol
Madini, Fahari Yetu
Bia yenye nguvu zaidi, inayowakilisha uthubutu, kazi na fahari ya Watanzania, hususan wale wanaothamini ladha nzito na vionjo vya kipekee.Mafanikio haya yanaonesha dhamira ya dhati ya kampuni kumpatia Mtanzania vinywaji vya viwango vya kimataifa kwa bei nafuu, huku ikisisitiza matumizi ya kistaarabu kwa watu wa miaka 18 na zaidi.
KIWEZESHI CHA MAFANIKIO
Mafanikio ya East African Spirits (T) Ltd yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji mkubwa katika teknolojia na rasilimali watu, ikiwemo:
- Matumizi ya mitambo
ya kisasa ya charcoalation katika kusafisha pombe kali ili kupata
kinywaji laini na safi.
- Crossflow filtration katika uchujaji wa bia, inayohakikisha ubora na
usalama wa bidhaa.
- Ushirikiano na wataalamu
waliobobea kimataifa, akiwemo Brewmaster mwenye heshima duniani.
- Matumizi ya malighafi bora kama:
- Kimea cha shayiri kutoka Ujerumani
- Shayiri, mchele na mahindi kutoka Tanzania
- Maji safi yanayochakatwa kitaalamu kwa uwiano sahihi
wa madini
AHADI KWA WATANZANIA NA DUNIA
East African Spirits (T) Ltd inaendelea kuahidi Watanzania na soko la kimataifa kuwa itaendelea kuwa mstari wa mbele katika ubunifu, ubora na uzalishaji wa vinywaji vyenye hadhi ya kimataifa, huku ikizingatia mahitaji ya soko na ustawi wa jamii.
Kupitia uwekezaji huu, East African Spirits (T) Ltd inatoa wito kwa Watanzania kuendelea kuunga mkono bidhaa za ndani, kama njia ya kukuza uchumi wa taifa, kuimarisha sekta ya viwanda na kuacha alama chanya kwa vizazi vijavyo.
Tumia vya kwetu – tujenge vyetu kwa ajili ya vizazi vyetu!
MAWASILIANO YA KAMPUNI
EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD
Makao Makuu: P.O. Box 707, Shinyanga, Tanzania
π +255 767 650 806
π +255 652 096 254
π§ info@eastafricanspirits.com- Hanson’s Choice Brandy
π₯πΆ TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

















Post a Comment