" Gerson Msigwa “Tunasubiri Majibu ya IshowSpeed Kuhusu Kuja Tanzania”, ( Ni kweli atakuja? )

Gerson Msigwa “Tunasubiri Majibu ya IshowSpeed Kuhusu Kuja Tanzania”, ( Ni kweli atakuja? )

 

Baada ya maswali na hisia mbalimbali kuibuka mitandaoni kuhusu kwa nini IShowSpeed hajafika nchini Tanzania licha ya ziara yake ya “Speed Does Africa Tour”, msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi na kusema kuna juhudi zinaendelea kuhakikisha anatembelea taifa hili.

“Tuliwasiliana na menejimenti yake na tunaamini ukaribisho wetu unaendelea kufanyiwa kazi. Tulimuandikia na tunasubiri majibu atueleze lini atakuja Tanzania. Tunaamini ni ziara muhimu kwa kutangaza fursa zetu za utalii, kuitangaza nchi yetu na kuambia dunia uhalisia wa Tanzania,” amesema Gerson Msigwa.

Kauli hiyo imejiri wakati IShowSpeed akiendelea na ziara yake ya livestream barani Afrika ambapo tayari ametembelea Kenya, huku akitangaza kuwa ziara hiyo itamfikisha kwenye nchi 20.

Hadi sasa, Tanzania haijatajwa rasmi kama moja ya nchi atakazotembelea, lakini matarajio bado yapo.

Post a Comment

Previous Post Next Post