Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, leo Jumanne Januari 27, 2026 ameshiriki kikamilifu zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Manispaa ya Mpanda, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kulinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ndugu Maduka ameshiriki zoezi hilo kwa niaba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Ndugu Musa Ramadhan Mwevi, katika zoezi lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bi. Jamila Yusuph.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bi. Jamila Yusuph, ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa Wilaya ya Mpanda kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili waendelee na masomo ya elimu ya msingi na sekondari.
Amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuwa balozi wa elimu kwa kuhamasisha jamii nyumba kwa nyumba kuhusu suala la elimu.
Zoezi la upandaji miti limeelezwa kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha utunzaji wa mazingira, kuendeleza rasilimali asilia pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanajamii katika kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha, zoezi hilo limefanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo limechukuliwa kama ishara ya heshima, uzalendo, mshikamano na upendo kwa kiongozi mkuu wa nchi.
Kauli mbiu ya zoezi hilo ilikuwa:
“UZALENDO NI KUTUNZA MAZINGIRA, SHIRIKI KUPANDA MITI.”
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Bi. Jamila Yusuph akiongoza zoezi la upandaji miti.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka, akishiriki zoezi la upandaji miti.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Ndugu Jimotoli Jilala Maduka.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment