MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.
......
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuanzisha na kuendeleza kongani za viwanda kupitia taasisi zake, hatua inayochochea fursa za ajira na ukuaji wa uchumi nchini.
Akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwanyika,amesema usimamizi madhubuti wa Wizara katika miradi ya kimkakati na miradi kielelezo kuwa kinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kubadili sura ya sekta ya viwanda.
"Miradi hiyo inapaswa kutekelezwa mapema iwezekanavyo kwa kuwa ina mchango muhimu katika kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi wa viwanda kwa ujumla."amesema Mhe.Mwanyika
Aidha, ameisisitiza Wizara kuendelea kuboresha sera na sheria ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na hivyo kuweka msingi wa uchumi shindani, jumuishi na shindanishi.
Kwa upande wao, Wajumbe wa Kamati hiyo wamepongeza juhudi za Wizara na kutoa mapendekezo mbalimbali ya kuboresha zaidi maendeleo ya sekta ya viwanda na biashara, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Wizara hiyo kuhakikisha mageuzi yanayolenga ukuaji wa kasi wa sekta yanatekelezwa ipasavyo.
Awali, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, akijibu hoja na maoni ya wajumbe , ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara itaendeleza ushirikiano makini katika kuimarisha sekta ya viwanda na biashara, ikijikita katika uanzishaji wa kongani mpya za viwanda zinazochochea ajira, ufufuaji wa viwanda vilivyokuwa vimesimama, kuongeza uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa, pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji leseni za biashara.
Ameongeza kuwa Wizara imeweka kipaumbele katika usimamizi wa miradi ya kimkakati na miradi kielelezo kwa weledi, ubunifu na umakini mkubwa, ikiwemo Mradi wa Liganga na Mchuchuma ambao una mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya viwanda, ujenzi wa uchumi wa taifa na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa malighafi za chuma kutoka nje ya nchi.

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri,akichangia mada katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo,wakichangia mada mbalimbali wakati wa kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, akijibu hoja na maoni ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo mara baada ya kamati hiyo kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, akitoa maoni ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo mara baada ya kamati hiyo kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma.

Post a Comment