" MABIGWA WATETEZI AFCON 2025 WAAGA MASHINDANO

MABIGWA WATETEZI AFCON 2025 WAAGA MASHINDANO






Mabingwa watetezi wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Ivory Coast wametolewa nje ya mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Misri (Egypt) katika mchezo wa robo fainali uliochezwa  Januari 10, 2026 nchini Morocco.

Katika mchezo mwingine wa robo fainali, Nigeria imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Algeria kwa mabao 2-0.

Kwa matokeo hayo, katika hatua ya nusu fainali kwanza Senegal watakutana na Misri, mchezo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizo mbili barani Afrika.

Nusu fainali ya pili Nigeria watachuana na na wenyeji wa michuano hiyo Morocco, michezo ambayo yote itachezwa siku ya jumatano ya tarehe 14/1/2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post