" MHE. PENDO AWATAKA WAKANDARASI KUIPA KIPAUMBELE MIRADI YA ELIMU.

MHE. PENDO AWATAKA WAKANDARASI KUIPA KIPAUMBELE MIRADI YA ELIMU.

Na. Elias Gamaya - SHINYANGA

Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Pendo John Sawa, amewataka
 wakandarasi wa Halmashauri kuipa kipaumbele miradi yenye uhitaji mkubwa kwa wananchi, hususan miradi ya elimu, ili ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma bora kwa wanafunzi.

Mhe. Pendo ametoa wito huo leo Januari21, 2026, wakati wa ziara ya Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Manispaa kwa lengo la kujionea hali ya utekelezaji na maendeleo yake.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Pendo Amesema kuwa miradi yote inayotekelezwa ina umuhimu mkubwa kwa jamii, hata hivyo ni vyema kuweka mkazo zaidi katika miradi inayohitaji kukamilika kwa haraka, hasa miradi ya shule, ili kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora, salama na rafiki zaidi ya kujifunzia.

“Miradi yote ni muhimu kwa jamii yetu, lakini tunapaswa kuwa makini zaidi na miradi yenye uhitaji wa haraka hususan shule, ili watoto wetu wapate maeneo mazuri na bora ya kusomea,” amesema Mhe. Pendo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Peres Kamugisha, amesema Menejimenti ya Manispaa ipo tayari kupokea ushauri wa Kamati ya Fedha pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuboresha miundombinu na huduma zinazotolewa kwa wananchi, sambamba na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora katika mazingira salama.

“Menejimenti ya Manispaa ya Shinyanga ipo tayari kupokea ushauri muda wowote kutoka kwa wananchi na Waheshimiwa Madiwani ili kuendelea kuboresha Manispaa kupitia utekelezaji wa miradi katika kata zote,” amesema Ndg. Kamugisha.
Nao baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wameipongeza Menejimenti ya Halmashauri kwa juhudi zake za kuendeleza kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Fedha ya Manispaa ya Shinyanga imetembelea miradi mitano (05) ikiwemo ujenzi wa Shule Mpya ya Butulwa kata ya Old Shinyanga, ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Bugayambelele kata ya Kizumbi, ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi kata ya Lubaga, ukarabati wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Mwamapalala kata ya Chibe, pamoja na kukagua ujenzi wa Stendi Mpya ya Mabasi ya Mikoa Katunda kata ya Kizumbi.













 

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post