" Mkubwa Fella: "Nikifa Msije Mkang’ang’ania Jeneza Langu Kunipeleka Leaders”

Mkubwa Fella: "Nikifa Msije Mkang’ang’ania Jeneza Langu Kunipeleka Leaders”

 


Hivi sasa Meneja wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella, anaumwa. Hali yake imezua hisia tofauti mitandaoni, hasa baada ya mke wake kufunguka na kudai kuwa wasanii aliowasaidia kwa muda mrefu wamemtupa na hawajamsaidia chochote katika kipindi hiki kigumu.

Sakata hili limepelekea mgawanyiko wa pande mbili, upande mmoja unaoongozwa na Dudu Baya unadai kuwa Mkubwa Fella aliwahi kunufaika sana kupitia wasanii, kisha akawanyonya hivyo hastahili msaada wowote; huku upande mwingine unaoongozwa na Mwijaku ukisisitiza kuwa yaliyopita si ndwele, kinachotakiwa sasa ni kumsaidia kwa hali na mali kwani afya yake ni muhimu zaidi.

Kufuatia mjadala huo, imeibuka tena clip ya miaka kadhaa iliyopita ambapo Mkubwa Fella anatoa onyo kuwa siku akifa, watu wasijifanye kulia au kung’ang’ania jeneza lake kulipeleka Leaders Club kwa maombolezo makubwa, ilhali kwa sasa hawathamini wala kutambua mchango wake.

Ikumbukwe kuwa Mkubwa Fella ndiye meneja wa kwanza mkubwa wa wasanii nchini Tanzania na ametengeneza njia kwa mamia ya wasanii, zaidi ya 100 kati yao wakitoka mikononi mwake.

Kiukweli sakata la Fella linasikitisha sana lakini hatuna budii kumbuka wale walioweka misingi ya mafanikio ya wengine, tuachane na hadithi zisizokuwa na ushahidi kuwa alinyonya wasanii bali tuungane pamoja kumuombea na kusaidia matibabu yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post