" Mzamiru Yassin Aikimbia SIMBA na Kujiunga na TRA SPORTS CLUB

Mzamiru Yassin Aikimbia SIMBA na Kujiunga na TRA SPORTS CLUB

 

Mzamiru Yassin (30), amejiunga rasmi na TRA United kwa mkataba wa miaka miwili.

Mzamiru ambaye alikuwa amebakiwa na miezi sita kwenye mkataba wake, aliomba kuachwa na Simba SC katika dirisha hili la usajili la Januari 2026 kwa lengo la kutafuta changamoto mpya na kupata nafasi zaidi ya kucheza ili kulinda na kuendeleza kiwango chake.

Anaondoka Simba SC baada ya kutumikia Wekundu wa Msimbazi kwa zaidi ya muongo mmoja, tangu Julai 1, 2016 hadi Januari 2026.

Tunamshukuru kwa mchango wake mkubwa ndani ya klabu na tunamtakia kila la kheri katika safari yake mpya.

Post a Comment

Previous Post Next Post