" NECTA YATANGAZA MATOKEO YA UPIMAJI WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI 2025

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA UPIMAJI WA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI 2025

 





MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2025



MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2025

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa darasa la nne ambapo ufaulu umepanda kwa asilimia 2.67 na asilimia 88 ya wanafunzi wamefaulu na kidato cha pili.

Matokeo yametangazwa leo Januari 10, 2026 na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohamed, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mtihani wa upimaji wa kidato cha pili jumla ya wanafunzi 898,718 walisajiliwa wakiwemo wasichana 497,891 sawa na asilimia 55.48 na wavulana 400,827 sawa na asilimia 44.5.

Waliofanya mtihani huo walikuwa wanafunzi 811,575 sawa na asilimia 91.3 katika shule za sekondari 6,223. Aidha wanafunzi 77,689 sawa na asilimia 8.7 hawakufanya upimaji huo pamoja na kuwa walisajili.

Jumla ya wanafunzi 1,583,686 walisajiliwa kufanya mtihani wa upimaji wa darasa la nne wakiwemo wasichana 818,673 sawa na asilimia 52 na wavulana 765,013 sawa na asilimia 48.

Mahudhurio ya wanafunzi wa darasa la nne yalikua asilimia 94 sawa na wanafunzi 1,490, 377 katika shule za msingi 20,508 ambapo ufaulu kwa wasichana wamefaulu kwa asilimia 53 huku wavulana ikiwa asilimia 47.

Aidha, wapo wanafunzi 93,309 sawa na asilimia 6 ambao hawakufanya mtihani huo pamoja na kuwa walisajiliwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post