Na Mwandishi wetu, Misalaba Media Mrisho Ngasa, mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na vilabu vikubwa vya Yanga, Simba na Azam FC, amewasili leo tarehe 30/01/2026 mkoani Ruvuma, tayari kwa ajili ya uzinduzi wa mashindano ya WAILES SUPER CUP yatakayofanyika wilayani Mbinga. Ujio wake umevutia hisia za wadau wa michezo na vijana wengi wanaopenda soka katika wilaya hiyo.Akizungumza mara baada ya kuwasili, Ngasa amesema lengo kuu la mashindano hayo ni kuhakikisha kunakuwepo na uibuaji wa vipaji vipya vya soka kutoka ngazi ya chini. Ameeleza kuwa uzinduzi wa mashindano hayo kesho utakuwa fursa muhimu ya kuwaona na kuwachambua wachezaji wenye vipaji ambavyo bado havijapata nafasi ya kuonekana katika majukwaa makubwa.Ngasa ameongeza kuwa wachezaji watakaobainika kuwa na uwezo mkubwa watachukuliwa na kujiunga na kituo chake cha Enjoy Soka, ambacho kinalenga kulea na kukuza vipaji vya vijana ili waweze kufikia ngazi za juu zaidi za soka kitaifa na kimataifa.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment