Na Ngonise Kahise, Misalaba Media -Dar Es Salaam Tanzania imeanza safari ya kujiweka kwenye ramani ya kimataifa ya matibabu ya saratani, kufuatia hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) ili iwe kitovu cha tiba ya saratani Afrika Mashariki.Akizungumza Januari 5,2026 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya ORCI jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inalenga kuifanya ORCI kuwa kituo cha ubora wa matibabu ya saratani kitakachohudumia wagonjwa wa ndani na wale kutoka nchi jirani. “Dira yetu ni kuijenga ORCI iwe taasisi ya mfano barani Afrika, na ndani ya miaka mitatu hakuna Mtanzania anayepaswa kwenda nje ya nchi kutibiwa saratani,” alisema.Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa uwekezaji unaoendelea kufanywa katika miundombinu, teknolojia za kisasa na rasilimali watu ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya kuboresha huduma za saratani.“Chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imepiga hatua kubwa na sasa ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye uwezo wa kutoa huduma za kisasa za uchunguzi na matibabu ya saratani.”AmeelezaKabla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Waziri amekagua miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ufungaji wa mashine tatu mpya za tiba ya mionzi aina ya LINAC na Cobalt, upatikanaji wa mashine za kisasa za uchunguzi na matibabu ikiwemo PET CT, pamoja na uanzishaji wa kinu cha kuzalisha dawa za nyuklia (Cyclotron) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.Aidha, amekagua ujenzi wa jengo jipya la huduma za kimataifa linalolenga kuboresha huduma kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi, hatua inayotarajiwa kuongeza hadhi ya ORCI katika kutoa huduma za rufaa za kimataifa. Pia ameipongeza Menejimenti ya ORCI kwa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa Desemba 2025 ya kuhakikisha mashine tatu za PET zinafungwa na kuanza kutoa huduma.Katika ziara hiyo, Waziri Mchengerwa amezungumza na wagonjwa waliokuwa wakipatiwa huduma, ambapo kwa niaba yao Bi. Justina Allen amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za tiba ya mionzi. “Kwa sasa wagonjwa wasio na uwezo wanapata matibabu bure baada ya kufuata taratibu zilizowekwa, jambo ambalo limetupa matumaini makubwa,” amesema JustinaHata hivyo, Waziri Mchengerwa amesisitiza kuwa mageuzi ya huduma za saratani hayaishii kwenye majengo au mashine pekee. “Tunataka mageuzi yaanze kwenye usanifu wa utoaji huduma, matumizi ya teknolojia za kisasa, mifumo ya kielektroniki ya taarifa za wagonjwa na uzoefu wa mgonjwa kwa ujumla,” Vilevile Mchengerwa amesisitiza kuwa ORCI inapaswa kuwa bunifu, jasiri na kuimarisha utafiti pamoja na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa ili kuwa kituo kinachoongoza katika matibabu na utafiti wa saratani Afrika Mashariki.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dkt. Diwani Msemo, amesema kukamilika kwa ufungaji wa mashine mpya kutapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusubiri huduma. “Muda wa kusubiri utapungua kutoka wiki 20 hadi takribani wiki mbili, huku idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kwa siku ikiongezeka kutoka 200 hadi zaidi ya 400,” amesema Msemo

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment