Ombi hilo limetolewa leo Jumamosi Januari 24, 2026 na Mkurugenzi wa BMG Media, George Binagi wakati wa hafla fupi ya kupokea tuzo maalum kutoka YouTube baada ya BMG Media kufikisha wafuasi (subscribers) laki moja.Binagi amesema licha ya Serikali kupunguza gharama za usajili wa online media kutoka shilingi milioni moja hadi laki tano, bado wanaomba Serikali kushusha gharama hizo hadi laki moja hatua itakayosaidia vijana wakiwemo wahitimu wa uandishi wa habari kujiajiri.Pia amesema kuanzia mwaka huu 2026 watengeneza maudhui mtandaoni wameanza kukatwa asilimia tano ya mapatano wanayopata mtandaoni na kuwasilishwa serikalini wakati huo huo wakilipa kodi jambo ambalo limewaongezea mzigo wa kulipa kodi mara mbili na hivyo kuomba suala hilo kutatuliwa.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa MISATAN na MPC, Edwin Soko amesema mitandao ya kijamii kwa sasa ni fursa kwa vijana kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini, hivyo amehimiza matumizi sahihi ya mitandao hiyo.Kuhusu gharama za usajili na kodi mbalimbali, Soko amesema atafikisha suala hilo kwa mamlaka husika kupitia vikao mbalimbali vya wadau wa habari ambavyo vimekuwa vikifanyika kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment