Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoa wa Mbeya, Bi. Agness Bashemu.Na Lydia Lugakila -Misalaba MediaMbeyaKatibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoa wa Mbeya, Bi. Agness Bashemu, ameendesha semina maalum ya uongozi kwa viongozi na watendaji wa UWT mkoani humo, iliyolenga kuwajengea uwezo na kuwakumbusha misingi na sifa za kiongozi bora, hatua iliyowafanya baadhi ya viongozi kukiri kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku huku akipongezwa kwa mafunzo hayo. Semina hiyo ilifanyika Januari 28, 2026 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya iliwahusisha viongozi na watendaji wa UWT, madiwani wa viti maalum pamoja na madiwani wanawake wa kata mbalimbali za Mkoa wa Mbeya.Akizungumza wakati wa semina hiyo, Bi. Bashemu alieleza kuwa kiongozi bora anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa tabia, mienendo, hulka, bidii pamoja na uvaaji unaoendana na nafasi yake ya uongozi.Alisisitiza umuhimu wa kiongozi kuwa karibu na watu anaowaongoza, kujitambua, kujifahamu uwezo wake, kutambua sifa zake chanya pamoja na changamoto anazokabiliana nazo katika uongozi.Aidha, Bi. Bashemu alibainisha kuwa kiongozi ni lazima awe mtu anayemcha Mungu, anayezingatia maadili ya dini yake, pamoja na kujenga na kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa viongozi wenzake.Aliongeza kuwa kiongozi bora ni yule anayejali makundi maalum katika jamii yakiwemo watu wenye ulemavu, wagonjwa waliopata ajali, wajane wasio na uwezo, wazee na vikongwe.Katibu huyo wa UWT Mkoa alisisitiza kuwa kiongozi anatakiwa kuwaheshimu viongozi wenzake bila kujali ngazi zao, kuwapenda, kuwajali na kuwaheshimu watu anaowaongoza bila chuki wala upendeleo.Bashemu alifafanua kuwa kiongozi wa haki ni yule anayesimamia ukweli, kuwatetea na kuwasemea watu wake bila woga, pamoja na kuheshimu maamuzi ya vikao halali hata kama hakushiriki katika vikao hivyo.Pia aliwakumbusha viongozi umuhimu wa kujiandaa kabla ya mikutano na vikao kwa kuandaa hoja au hotuba, badala ya kuwa walopokaji wasio na maandalizi.Bi. Bashemu alisisitiza umuhimu wa kiongozi kukiri makosa, kukubali kukosolewa na kuomba msamaha pale inapobidi, pamoja na kutunza siri za vikao na za watu wengine, akionya kuwa kiongozi asiyeweza kutunza siri si muadilifu.“Kila kitu chako kikiwa wazi ni sawa na kujivua nguo,” alisema Bi. Bashemu, huku akisisitiza kuwa kiongozi anatakiwa kumtambua mwenza wake wa ndoa kama sehemu ya uongozi wake.Kwa upande mwingine, aliwakumbusha viongozi umuhimu wa kuheshimu muda wao na wa watu wengine, akibainisha kuwa nidhamu ya muda ni nguzo muhimu ya uongozi bora.Semina hiyo ilihitimishwa kwa viongozi kutoa shukrani na zawadi kwa mwezeshaji huyo ikiwa ni ishara ya kuthamini mafunzo waliyopata na dhamira yao ya kuboresha utendaji wao wa uongozi.
Katibu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoa wa Mbeya, Bi. Agness Bashemu, akizungumza.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment