Na Mwandishi wetu, Misalaba Media Wananchi katika Mtaa wa Nyamagana Jijini Mwanza wamepongeza kuanza kwa ujenzi wa Daraja la Uhuru lilokuwa likileta changamoto ya kujaa Maji juu yake na hivyo kuzuia magari na watembea kwa miguu.Mwananchi aishiye Mtaa wa Uhuru Marco Lucas alisema wamefurahishwa kuanza kwa ujenzi wa Daraja Hilo lilokuwa kero nyakati za Mvua kwani Maji yalikuwa yakipita juu na kuathiri kupita kwa magari na Kusababisha vifo vya watu.Alisema anaipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuanza kujenga daraja hilo kuwaondolea wananchi adha ya kukabiliana na mafuriko kipindi cha Mvua kutokana na Daraja kushindwa kupitisha Maji hivyo kusambaa na kufikia kwenye Nyumba.Naye Diwani wa Kata ya Nyamagana, Frank Chacha alishukuru kuanza kwa ujenzi wa Daraja Hilo ili kuweza kuondoa adha ya Muda Mrefu ambayo imewakumba wananchi kwenye eneo Hilo.Alisema Shughuli zilizofanywa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini Tanzania (TARURA) za kuinua Daraja Hilo kuwezesha kupitisha Maji vizuri ni za kupongezwa kwani hakutakuwa na kukwama tena kupita kwa Maji.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment