" WAZIRI AWESO: SH. TRILIONI 3 ZATUMIKA KUTATUA KERO YA MAJI, VIJIJI 10,758 VYANUFAIKA

WAZIRI AWESO: SH. TRILIONI 3 ZATUMIKA KUTATUA KERO YA MAJI, VIJIJI 10,758 VYANUFAIKA


Na. Meleka Kulwa, Dodoma

‎Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutekeleza kikamilifu ahadi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kero ya maji nchini inamalizwa, akitoa taarifa hiyo kwa umma tarehe 28 Januari 2025 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

‎Amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne, jumla ya shilingi trilioni 3 zimetumika katika sekta ya maji nchini, ikiwa ni jitihada za makusudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

‎Aidha amebainisha kuwa kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi trilioni 1.8 kimeelekezwa maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

‎Amesema kuwa kati ya vijiji 12,333 vilivyopo nchini, Serikali imeshafikisha huduma ya maji katika vijiji 10,758.

‎Aidha amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka minne pekee ya uongozi wa Rais Samia, vijiji 7,929 vimefanikiwa kufikiwa na huduma ya maji, jambo ambalo ni rekodi ya kipekee.

‎Amesema kuwa kwa sasa vimebaki vijiji 1,575 tu nchi nzima ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya maji.

‎Waziri Aweso amesema kuwa Wizara ya Maji haitalala mpaka vijiji vyote vilivyobaki 1,575 vipate huduma ya maji safi na salama.

‎Aidha amebainisha kuwa kuanzishwa kwa RUWASA imekuwa mkombozi mkubwa katika kusimamia miradi ya maji vijijini na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa wananchi wa hali ya chini.

‎Amesema kuwa mabadiliko hayo ya kimkakati yameifanya Wizara ya Maji kutoka kuwa wizara ya malalamiko na sasa kuwa wizara ya utekelezaji na matokeo.










Post a Comment

Previous Post Next Post