" WAZIRI MCHENGERWA AMWAGIA SIFA KITUO CHA AFYA KALOLENI.

WAZIRI MCHENGERWA AMWAGIA SIFA KITUO CHA AFYA KALOLENI.

 Na Egdia Vedasto, Misalaba Media,

Arusha

Waziri wa afya Mohamed Mchengerwa amemwaga sifa kwa kituo cha afya Kaloleni kilichopo Jijini Arusha baada ya kukagua na kujiridhisha uwepo wa vifaa tiba vya kisasa na huduma safi kutoka kwa watumishi.


Amesema hayo katika ziara yake aliyoifanya katika kituo cha afya Kaloleni na kupongeza utendaji was watumishi wa afya was kituo hicho wakiongozwa na Mganga mfawidhi Dr.Anna Kimaro.


Aidha Mchengerwa ametoa maelekezo kyanza Mara moja kwa ujenzi wa jengo la ghorofa ili kuhakikisha msongamano wa wagonjwa unaisha.

Hata hivyo kufuatia upungufu wa watumishi wa afya katika kituo hicho ameagiza halmashauri ya jiji la Arusha kwa kutumia mapato ya ndani kuajiri watumishi wa kujitolea kwa muda wakati ambapo serikali inaendelea kutoa ajira za kudumu.

Katika namna hiyo hiyo ametoa marufuku ya wagonjwa kununua dawa mitaani nje ya vituo vya afya ilihali dawa zimejaa bohari ya dawa (MSD)


Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kaloleni Dr.Anna Kimaro amesema kituo kimeendelea kupiga hatua za kiutendaji kwa kuhakikisha kinasimika vifaa tiba vya kisasa, lengo likiwa ni kuhakikisha wateja wanapata huduma ya uhakika na kwa karibu.

"Kutokana na mapato ya ndni ya halmashauri yetu tumefnukiwa kununua machine ya kisasa ya kuchunguza magonjwa ya ndani ikiwemo saratani ya matiti iliyogharimu zaidi ya milioni mia nne na kuokoa maisha ya wanawake kwa kiasi kikubwa",

" Malengo yetu ni kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wengi na kwa wakati, kwa kutumia vifaa vya kisasa na kuokoa maisha ya wananchi wetu" amesema Dr.Anna.


Vilevile Mkururgenzi wa jiji LA Arusha John Kayombo amesema amepokea maelekezo ya Waziri wa Afya na tayari mikakati ya kujenga jengo la ghorofa ili kupanua wigo wa huduma zetu.

"Tutatumia mapato yetu ya ndani kukamilisha jengo hili kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika kituo hiki na vinginevyo vilivyomo ndani ya Jiji" amesema Kayombo.

Vilevile Mganga mkuu wa halmashauri ya jiji LA Arusha Dr Maduhu Nindwa amesema uwekezaji katika kituo hicho mefabyika wa kina na kugharimu zaidi ya bilioni 11.

  

Post a Comment

Previous Post Next Post