
Na Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ametoa maagizo kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ghorofa katika Kituo cha Afya Kaloleni, hatua inayolenga kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma katika kituo hicho.
Akizungumza jiji Arusha wakati wa ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho, Waziri Mchengerwa amesema ongezeko la wagonjwa limefanya miundombinu iliyopo kushindwa kukidhi mahitaji, hivyo ujenzi wa gorofa ni hatua muhimu ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi.
Aidha Waziri Mchengerwa amefurahishwa na utendaji kazi wa baadhi ya watoa huduma katika kituo hicho, akiwemo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kaloleni,Dokta Anna Simon Kimaro kwa juhudi zao za kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati licha ya changamoto zilizopo.
Aidha, Waziri Mchengerwa amesema ni lazima huduma zote za dawa zipatikane ndani ya kituo hicho, huku akisisitiza kuwa hakuna mgonjwa anayepaswa kupelekwa kununua dawa nje ya kituo, kinyume na maelekezo ya serikali.
Waziri Mchengerwa amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji na utu kwa wahudumu wa afya, akiwataka kuzingatia maadili ya kazi na kutumia lugha nzuri na yenye staha kwa wagonjwa, kwani huduma bora huanza na mawasiliano mazuri.
Ameongeza kuwa, endapo ujenzi wa kituo hicho cha afya utakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa, Serikali itaipandisha hadhi Kituo cha Afya Kaloleni kuwa Hospitali ya Wilaya, kutokana na sifa zake za kuwa na vifaa vya kisasa na uwezo wa kutoa huduma zote muhimu za afya.
Aidha ameitaka halmashauri ya jiji la Arusha kuhakisha wanaanza mapema ujenzi na kutafuta eneo mbadala la kuweza kujenga kituo kingine Cha Afya kitakachoweza kubeba wagonjwa ili kuweza kuwapunguzia foleni kituo Cha Afya Kaloleni.
Aidha waziri wa Afya amemtaka Katibu mkuu wa wizara ya Afya ambaye alikuwa ameambatana naye kuhakisha anaondoa duka la dawa nje ya hospitali ya wilaya ya Temeke linalomilikiwa na Daktari wa hospitali hiyo.
Pamoja na hayo yote Waziri wa Afya baada ya kuridhishwa na uendelezaji wa kituo ca Afya Kaloleni kwa kuweza kununua vifaa vya vipimo zaidi ya hospitali ya wilaya vyenye zaidi ya gharama ya Bilioni 1.16 na kutaka ikikamilisha majengo kupewa hadhi ya kuwa hospitali ya wilaya.



🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment