" Zifahamu Lugha Zinazozungumzwa zaidi Duniani

Zifahamu Lugha Zinazozungumzwa zaidi Duniani

 

KIINGEREZA kimeendelea kuwa lugha yenye ushawishi mkubwa duniani, ikitajwa kuwa ndiyo iliyokuwa na wazungumzaji wengi zaidi kwa mwaka 2025.

Ni kwa mujibu wa utafiti wa tovuti maarufu ya takwimu ya Visual Capitalist, ambayo imekitaja Kiingereza kuwa na wazungumzaji bilioni 1.5.

Mafanikio hao ya Kiingereza yanatokana na namna lugha hiyo inavyotumika katika masuala ya biashara, mawasiliano ya kimatafa na uchumi wa kidigitali.

Lugha ya pili iliyoongoza kwa kuwa na wazungumzaji wengi mwaka 2025 ni Kichina. Wazungumzaji bilioni 1.1.

Kichina kimeshika nafasi hiyo kutokana na idadi kubwa ya raia wake, pia kwa ushawishi wake mkubwa kimataifa katika miaka ya hivi karibuni.

Lugha ya Kihindi inafuata katika nafasi ya tatu, ambapo kwa mwaka 2025 ilikuwa na wazungumzaji milioni 609. Wakati huo huo, Kihispania kimeshika nafasi ya nne kikiwa na wazungumzaji takribani milioni 558 kwa mwaka 2025.

Kuenea kwa lugha hiyo kumetokana na kutumiwa si tu Hispania, bali pia katika maeneo ya Latin ya Amerika na baadhi ya majimbo nchini Marekani.

Lugha zingine zinazokamilisha ‘Top 10’ ya zile zilizokuwa na wazungumzaji wengi mwaka 2025 ni Kiarabu, Kifaransa, Kibengali, Kireno, Kirusi na Kiindonesia. Kila moja ina wazungumzaji zaidi ya milioni 250 duniani kote.

Post a Comment

Previous Post Next Post