Madereva wa Trekta wamepewa elimu ya kuzingatia Sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuacha kuendesha Trekta Kwa mazoea badala yake warudi vyuoni kupata elimu ya udereva ili kuepuka ajali wawapo barabarani.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewasisitiza madereva hao kukata leseni za udereva pindi wanapokamilisha mafunzo ya udereva ili kupata sifa ya kuingia na vyombo hivyo barabarani.Pamoja na hayo, Sajenti Ndimila amewaelimisha madereva hao kuacha kuendesha vyombo vilivyo vibovu ili kuepuka kuwa chanzo Cha ajali barabarani.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment