Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mbeya
Alex Mgaya (43), mkazi wa Mtaa wa Igodima, Kata ya Iganzo jijini Mbeya, anaomba msaada wa fedha kiasi cha shilingi milioni tatu (Tsh 3,000,000) kwa ajili ya matibabu ya macho katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Alex amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo kwa zaidi ya miaka sita sasa ambapo kipindi chote hicho, amefanyiwa matibabu katika hospitali mbalimbali bila mafanikio, hali iliyosababisha afya yake kuendelea kudorora.
Kutokana na changamoto hiyo, shughuli zake zote za kiuchumi zimesimama na biashara zake zimefilisika, jambo linalomfanya kushindwa kugharamia matibabu anayohitaji.
Kupitia waraka huu, Alex anawaomba Watanzania wenye uwezo kuguswa na hali yake na kumchangia ili aweze kupata matibabu stahiki.
Kwa mujibu wa Alex mtu yeyote atakayependa kutoa msaada anaweza kutuma mchango kupitia namba ya simu: 0754 353 839, jina: Alex Mgaya.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment