Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya Watu watatu akiwemo mwanaume mmoja na wanawake wawili wakazi wa Kitongoji cha Goye, Kijiji cha Goye, Kata ya Ndato, Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kubwa wakiwa wamejificha chini ya mti wa asili.Kwa mujibu wa ndugu wa familia, waliotajwa kufariki dunia ni Wilson Sanga (27), Sikuzani Tumaini Sanga (39) na Lucia Joseph Mlumbe (49).Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa saba mchana, Februari 19, 2026, wakati watatu hao walipokuwa wakivuna mahindi shambani. Mvua kubwa iliyoambatana na radi ilipoanza kunyesha, waliamua kujikinga chini ya mti wa asili, ndipo radi ilipowapiga na kusababisha vifo vyao papo hapo.Mwenyekiti wa Kitongoji alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji, ambaye aliarifu Jeshi la Polisi na kisha askari walifika eneo la tukio na kuuchukua miili ya marehemu na kuipeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Makandana, Tukuyu kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo.Taratibu za mazishi zinaendelea huku ikisubiriwa taarifa rasmi ya uthibitisho kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment