" MWILI WA MWANAFUNZI WA CBE MBEYA WAOPOLEWA KWENYE DIMBWI LA MAJI

MWILI WA MWANAFUNZI WA CBE MBEYA WAOPOLEWA KWENYE DIMBWI LA MAJI

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaMwanafunzi anayedaiwa kuwa wa Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, Tido Kadaga  mwenye umri miaka 20 amekutwa amefariki dunia baada ya mwili wake kuonekana ukielea kwenye dimbwi la maji katika Mtaa wa Maili Tano, Kata ya Iganzo, Jijini Mbeya huku chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika.Tukio hilo limetokea Februari 17, 2026 majira ya saa 8 mchana, baada ya baadhi ya mashuhuda na wasamaria wema kuliona dimbwi hilo likiwa na mwili ukielea juu ya maji na kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya.Akithibitisha tukio hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya, SSF Malumbo Ngata, amesema walipokea taarifa za uwepo wa mtu anayeelea kwenye dimbwi hilo, na walipofika eneo la tukio walikuta mwili huo ukiwa juu ya maji.Amesema baada ya kuuopoa mwili huo, ilibainika kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, aitwaye Tido Kadaga.Ameongeza kuwa Mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.“Bado hatujafahamu chanzo cha tukio hili tunaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kubaini sababu za kifo hicho" alisema Ngata. Mwili tumeupeleka Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa uchunguzi zaidi,” ameongeza Ngata.Aidha amewashukuru wasamaria wema waliotoa taarifa kwa wakati, na kutoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari hasa kipindi hiki cha mvua mkoani Mbeya.“Tunawaomba wananchi wawe waangalifu zaidi kipindi hiki cha mvua Wawaangalie watoto na wazee, na kuepuka kuvuka au kukanyaga madimbwi ya maji bila sababu za msingi,” ameonya.Alipotafutwa Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, Dk. Beny Mwenda, amesema wanasubiri taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi kabla ya kutoa ufafanuzi wa tukio hilo, na ameahidi kuzungumzia suala hilo mara baada ya kupokea taarifa hizo rasmi.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post