
Na Mapuli Kitina Misalaba
Katika kuadhimisha Siku ya Wapendanao, Mwenyekiti wa
Mtaa wa Bugweto A, Mary Makamba, ameambatana na wajumbe wa Serikali ya Mtaa huo
na kukabidhi msaada wa mashuka 60 kwa ajili ya wagonjwa katika Advent Health
Care Dispensary iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Bi. Mary Makamba
amesema ameamua kuitumia siku hiyo maalum ya wapendanao kwa kusaidia kutatua
changamoto za kijamii ndani ya mtaa wake, badala ya kuisherehekea kwa namna ya
kawaida.
Amesema zahanati hiyo ndiyo kituo kinachowahudumia
wananchi wa Bugweto A wanapokumbwa na changamoto za kiafya, wakifika kwa ajili
ya uchunguzi na matibabu ya awali, hivyo ni muhimu jamii kuendelea kuiunga
mkono ili iweze kutoa huduma bora zaidi.
Ametoa wito kwa wananchi na viongozi wengine kuiga
mfano huo kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji, hasa wagonjwa na makundi maalum,
ili kuifanya Siku ya Wapendanao kuwa na maana pana zaidi ya kijamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa zahanati hiyo ambaye
pia ni Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Lameck
Mihayo, ameishukuru Serikali ya Mtaa wa Bugweto A kwa msaada huo akisema
utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zinajitokeza hususan pale kunapokuwa
na wagonjwa wengi wanaohitaji huduma kwa wakati mmoja.
Amesema mashuka hayo yatasaidia kuboresha mazingira ya
huduma kwa wagonjwa na kuongeza faraja wanapokuwa wanapatiwa matibabu.

Bi. Mary Makamba (wa pili kutoka kushoto), Mwenyekiti
wa Mtaa wa Bugweto A, akikabidhi mashuka kwa madaktari wa Advent Health Care
Dispensary ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wapendanao.

Bi. Mary Makamba, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto A,
akiendelea kuuliza maswali na kupokea maelezo kutoka kwa wahudumu wa afya
kuhusu utoaji wa huduma katika Advent Health Care Dispensary iliyopo mtaa huo Manispaa
ya Shinyanga.

Bi. Mary Makamba, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugweto A,
akiendelea kuuliza maswali na kupokea maelezo kutoka kwa wahudumu wa afya
kuhusu utoaji wa huduma katika Advent Health Care Dispensary iliyopo mtaa huo Manispaa
ya Shinyanga.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment