" ULEVI SAFARINI WATAHADHARISHA USALAMA WA ABIRIA NA MADEREVA

ULEVI SAFARINI WATAHADHARISHA USALAMA WA ABIRIA NA MADEREVA



Abiria wanaosafiri masafa marefu nyakati za usiku wamepatiwa elimu ya kuheshimu Sheria za usalama barabarani wawapo ndani ya gari.

Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewataka Abiria kuacha tabia ya kunywa pombe kupita kiasi wawapo safarini kitu kinachowapelekea kuwa wasumbufu ndani ya Basi ikiwa ni pamoja na kumbugudhi dereva akiwa anaendesha gari.

Sajenti Ndimila amewaeleza Kuwa baadhi ya abiria wanaokuwa wamelewa wanakuwa na tabia ya kutaka kushuka kujisaidia mara kwa mara kisha kumsumbua dereva Kwa kauli za kukera kitu kinachompelekea dereva kukosa umakini akiwa anaendesha gari

Abiria wameaswa kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kukemea na kuzuia vitendo hivyo visitokee ndani ya gari hasa nyakati hizo za usiku kwani vitendo hivyo vinahatarisha usalama wa safari yao na watumiaji wengine wa barabara.

 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post