Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, Februari 11, 2026 amekutana na wananchi wa Kata ya Zongomela, Wilayani Kahama, kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za kiusalama zinazowakabili.Katika kikao hicho kilichofanyika Mtaa wa Dodoma, Kamanda Magomi alizungumza na wafanyabiashara mbalimbali na wananchi kwa ujumla, ambapo alipokea maoni, pamoja na mapendekezo yao kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo.Akizungumza na wananchi hao, SACP Magomi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu. Pia ameomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.Ziara hiyo ni mwendelezo wa utaratibu wa Kamanda huyo kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao, kusikiliza changamoto za kiusalama na kuzitatua kwa kushirikiana nao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment