
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Februari 11, 2026, kwenye Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni (KMC Complex), Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba SC walipata mabao yao mawili kupitia kwa mshambuliaji wao, Selemani Mwalimu, aliyefunga dakika ya 37, na Libasse Gueye aliyefunga dakika ya 45+4 katika kipindi cha kwanza.
Kufuatia matokeo hayo, Simba SC wamefikisha alama 19 baada ya kucheza mechi 8 na kushika nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwa upande mwingine, KMC wamebaki na alama 8 baada ya kucheza mechi 15, wakishika mkia katika msimamo wa ligi yenye jumla ya timu 16.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment