Abiria wa masafa marefu wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuacha tabia ya kutupa vitu dirishani wakiwa safarini.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa utupaji wa taka kama chupa za maji na mabaki ya vyakula unaweza kuhatarisha usalama Kwa watumiaji wengine wa barabara pia kumsababishia dereva wa gari nyingine kupoteza uelekeo na kusababisha ajaliAidha Sajenti Ndimila amewafahamisha kuwa utupaji wa taka dirishani unaweza kusababisha uharibifu wa vyombo vingine vya moto kama kupasuka kioo Kwa Magari mengine pia unaweza kusababisha majeruhi Kwa watembea Kwa miguu na madereva wa pikipiki.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment