" WAZIRI JOEL NANAUKA AZINDUA JUKWAA LA VIJANA MKOANI SHINYANGA, AWAHAKIKISHIA VIJANA FURSA

WAZIRI JOEL NANAUKA AZINDUA JUKWAA LA VIJANA MKOANI SHINYANGA, AWAHAKIKISHIA VIJANA FURSA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka amezindua rasmi Jukwaa la Vijana Mkoa wa Shinyanga, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Lyakale, Manispaa ya Shinyanga.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi binafsi pamoja na vijana kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga, waliokusanyika kwa lengo la kushuhudia hatua hiyo inayolenga kuimarisha ushiriki wa vijana katika maendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Nanauka amesema kupitia jukwaa hilo, Wizara itaimarisha mahusiano ya moja kwa moja kati ya Serikali na vijana, pamoja na kutoa taarifa sahihi kuhusu mikopo na mitaji inayotolewa kupitia mifuko ya serikali, programu wezeshi na taasisi za fedha.

Amesema lengo ni kuhakikisha vijana wanapata taarifa kwa wakati na wanachangamkia fursa zilizopo bila ya kuzunguka huku na kule.

“Tunataka katika miaka mitano ya Rais Samia, vijana wasihangaike kutafuta fursa, bali wao waamue wanataka fursa gani ili kuinua uchumi wao,” amesema.

Waziri Nanauka amesisitiza kuwa jukwaa hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana iliyorejewa na kuboreshwa mwaka 2024, inayolenga kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu katika maamuzi, wanapata ajira na fursa za ujasiliamali, wanakuwa wazalendo, wabunifu na kizazi chenye maadili.

Ameongeza kuwa jukwaa hilo linaendana na maono ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inayolenga kujenga Tanzania yenye uchumi shindani, unaojitegemea na unaotegemea viwanda, teknolojia na rasilimali watu wenye ujuzi.

“Ili kufikia lengo hilo vijana lazima wawe kitovu cha uzalishaji, wawe kitovu cha ubunifu na pia wawe sehemu ya uongozi wa taifa letu,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita amesema Mkoa umeendelea kuimarisha mazingira rafiki ya ujasiliamali kwa kusimamia miongozo na sera jumuishi zinazowawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Amesema hadi sasa jumla ya wafanyabiashara 2,453 wamesajiliwa kupitia juhudi za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kuratibu na kusimamia zoezi la usajili wa wajasiliamali.

RC Mhita amewahimiza vijana kutumia ipasavyo fursa zinazotolewa na Serikali, hususan wale wenye vipaji katika sekta mbalimbali.

Amesema si kila mtu ana kipaji, hivyo wenye vipaji wanapaswa kuvitambua na kuviendeleza kwa kufuata taratibu za usajili kupitia maafisa maendeleo na maafisa maendeleo ya vijana waliopo katika halmashauri.

Baadhi ya vijana waliohudhuria uzinduzi huo wameahidi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi na kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga.

Katika jukwaa hilo, mada na mijadala mbalimbali imewasilishwa, ambapo vijana wamejadili masuala ya ajira, ujasiliamali, mitaji, pamoja na namna ya kutumia teknolojia kama nyenzo ya kukuza uchumi wao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Febuari 21, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Febuari 21, 2026.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Dkt. Kedmon Mapana akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Vijana Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Febuari 21, 2026.



 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post