" ALONI ISHENGOMA KILOMBA KUNG’ARA RWAMISHENYE FESTIVAL 2026 KATIKA JUKWAA LA KUAMSHA FAHAMU NA MWELEKEO CHANYA KWA VIJANA

ALONI ISHENGOMA KILOMBA KUNG’ARA RWAMISHENYE FESTIVAL 2026 KATIKA JUKWAA LA KUAMSHA FAHAMU NA MWELEKEO CHANYA KWA VIJANA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Bukoba

Vijana wa Kata ya Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wameandaa jukwaa kubwa la Rwamishenye Festival 2026 lenye lengo la kuwaandaa vijana kujitambua, kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii na kuendana na mabadiliko ya ulimwengu wa sasa.

festival hiyo itakayofanyika Februari 7, 2026, siku ya Jumamosi, katika eneo la Kibila Plaza ambapo waandaaji wamemualika kijana maarufu na mchapakazi, Aloni Ishengoma Kilomba maarufu kama Gwayaka, kutoa mada maalum itakayolenga kuwajengea vijana misingi ya kufikiri chanya na kuwajibika katika jamii.

Akizungumza kuelekea tukio hilo, Aloni Ishengoma Kilomba amesema lengo lake kuu ni kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua, kujiamini na kufanya maamuzi sahihi yatakayowasaidia wao binafsi pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.

 Amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa na mtazamo chanya (positive attitude) ili waweze kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika mazingira yao.

Aloni, ambaye pia ni kijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema anajivunia kushiriki jukwaa hilo kwani linaendana na dhamira ya chama ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa jamii na maendeleo ya taifa kupitia kuimarisha maadili mema, mshikamano na uwajibikaji.

Aidha, amewahimiza vijana pamoja na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi na kutokukosa jukwaa hilo, akisema elimu itakayotolewa italeta mabadiliko chanya, kuongeza uelewa wa pamoja na kuwasaidia washiriki kuendana na mahitaji ya dunia ya sasa.

Mbali na mada ya elimu, Rwamishenye Festival 2026 itapambwa na shughuli mbalimbali za burudani na kijamii ikiwemo kukimbia kwa magunia, kukimbiza kuku, bonanza la mpira wa miguu, utoaji wa tuzo, kubadilishana mawazo pamoja na kupata chakula cha pamoja, hatua inayolenga kuimarisha mshikamano, umoja na ushirikiano miongoni mwa vijana na jamii kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post