Na:Belnardo Constantine, Misalaba Media.Askari Police mbalimbali kutoka Tanzania wakiwemo Maafisa,Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi nchini Tanzania ambao kundi linamaliza mda kuhudumu kulinda amani nchini Sudan kusini wamehitimisha kwa Paredi maalum ambayo ili ambatana na kuvishwa nishani( Medall Pin) kutambua kazi nzuri ya kulinda amani nchini humo.Duru zinasema Tanzania ni miongoni mwa nchi bora zinazochangia askari wake katika Operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa katika Baadhi ya mataifa barani Africa.Aidha, Miongoni mwa maafisa hao wamebainisha kuwa licha ya kuwepo mazingira magumu walijipa moyo kuendelea kulinda amani na kutoa elimu kwa makundi mengi zaidi.Sanjari na hilo wameendelea kuwashukuru Maafisa na Askari wa Majeshi mengine kwa namna walivyoshirikiana kudumisha amani katika misheni ya kulinda amani nchini Sudan Kusini.Vilevile wamewaomba wananchi wa Sudan kusini kuendelea kutunza na kulinda amani ya nchini hiyo
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment