Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media
Mwanasiasa mkongwe Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Said Ally Bungara(Bwege)
ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT Wazalendo kuanzia jana, Februari 18, 2026.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma, Bwege ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na hiyari yake mwenyewe kama mtu huru, baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kugundua kuwa ACT Wazalendo si
“rafiki sahihi” katika safari yake ya kisiasa kama
alivyokuwa amefikiria awali.
Bwege, ambaye anajulikana kwa msimamo wake thabiti na lugha za mvuto majukwaani, amebainisha kuwa mwelekeo wa sasa wa ACT Wazalendo ni tofauti na matarajio yake, jambo lililompelekea kuamua kutafuta jukwaa lingine la kuendeleza mapambano ya kisiasa.
“ACT Wazalendo si rafiki sahihi kwangu, nilivyofikiria ni tofauti na nilivyohisi. Kuanzia sasa mimi si mwanachama wa ACT Wazalendo tena kuanzia tarehe 18/2/2026.
Hatahivyo Mwanasiasa huyo amesema mambo menginie baadaye. "Ninategemea kushirikiana na kulitumia jukwaa la CHADEMA katika siasa za kudai demokrasia na maendeleo la taifa langu nilipendalo ka Tanzania”, Amesema
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment