Na Lydia Lugakila – KaragweDiwani wa Kata ya Rugera, Dawson Paul Byamanyirwohi, anatarajiwa kufanya sherehe maalum ya kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua tena kuwa diwani kwa awamu nyingine.Akizungumza na Misalaba Media, Diwani Byamanyirwohi amesema kuwa sherehe hiyo itafanyika Jumamosi, Februari 7, 2026, na itaambatana na maadhimisho ya miaka kumi na tano ya kuanzishwa rasmi kwa Kata ya Rugera, tangu mwaka 2010.Diwani huyo amewakaribisha wananchi wote wa Kata ya Rugera na maeneo jirani kushiriki katika tukio hilo muhimu, akisisitiza kuwa zawadi na michango mbalimbali vinakaribishwa kama sehemu ya kuunga mkono sherehe hiyo ya kihistoria.Sherehe hiyo inatarajiwa kuwa jukwaa la kuimarisha mshikamano kati ya viongozi na wananchi pamoja na kutathmini maendeleo ya kata hiyo tangu kuanzishwa kwake.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment