
Simba SC imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya Kombe la CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Greenland FC katika mchezo wa dakika 90 uliopigwa Uwanja wa Mej Isahmuyo.
Mnyama alianza vyema mchezo huo na kupata bao la kuongoza dakika ya 13 kupitia kwa Baraka Mwangosi, aliyenufaika na makosa ya mlinda mlango wa Greenland FC.
Katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake, kipa huyo alijikuta akipoteza umakini na mpira kumkuta Mwangosi ndani ya eneo la hatari (18), ambaye hakusita kuutumbukiza wavuni.
Dakika chache kabla ya mapumziko, Anthony Mligo aliwainua tena mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la pili dakika ya 45, akihitimisha kipindi cha kwanza kwa faida ya mabao mawili kwa sifuri.
Kipindi cha pili kilishuhudia mabadiliko kadhaa, huku Neo Maema aliyeingia akitokea benchi akihitimisha karamu ya mabao dakika ya 90 kwa kufunga bao la tatu, muda mfupi kabla ya filimbi ya mwisho.
Ushindi huo unaiondoa rasmi Greenland FC kwenye mashindano hayo, huku Simba SC ikiendelea na safari ya kusaka ubingwa kwa kusonga mbele hatua ya 32 bora.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment