Katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini jijini Dodoma hekima ya juu na hamu ya kudumisha amani ya taifa imetawala kufuatia kauli nzito ya Makamu wa Rais Daktari Emmanuel Nchimbi ambaye amewasihi Watanzania wote kuacha tabia ya kukumbushia matukio yaliyopita yaliyoleta simanzi kwa jamii.
Amesema hali hiyo itasaidia kuepuka kutonesha vidonda ambavyo vimeanza kupona. Alisema hayo kufuatia ushauri wa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika, Wakili Boniface Mwabukusi aliyesisitiza kuwa viongozi na wadau wa jamii wanapaswa kuwa na kiasi katika maneno yao ili kutochefua mioyo ya wananchi katika kipindi hiki ambacho taifa linahitaji utulivu na mshikamano kuliko wakati mwingine wowote.
Daktari Nchimbi amebainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wake tayari ameunda tume maalum ya kuchunguza ukweli wa mambo yote yaliyotokea wakati wa msimu wa uchaguzi mkuu uliopita na hivyo ni jambo la kiungwana na kisheria kusubiri matokeo ya tume hiyo badala ya kuendelea kutoa kauli zinazoweza kuathiri mchakato wa upatikanaji wa haki na amani ya kudumu.
Alisisistiza kwamba wote wanaoipenda Tanzania wanatakiwa kutoa nafasi kwa serikali kutimiza jukumu lake kwa weledi na uadilifu huku akisisitiza kuwa wito huo wa kutotonesha vidonda unawahusu pia wanasiasa wanaharakati na viongozi wa kijamii bila kubagua.
Upande wake Wakili Mwabukusi ameweka wazi kuwa uwazi na uwajibikaji ndiyo misingi itakayorejesha imani na matumaini ya wananchi kwa taasisi zao na kuimarisha taifa letu ambalo limepitia changamoto kubwa katika kipindi kilichopita huku akisisitiza kuwa TLS inatambua umuhimu wa hatua za kisheria zinazochukuliwa hivi sasa ili kuganga yajayo.
Mwelekeo huu wa viongozi wetu wa juu unatoa taswira njema kwa nchi yetu inayozidi kuaminika duniani kote kama kisiwa cha amani na utulivu kiasi cha kuvutia mikutano mikubwa ya kimataifa na watalii wanaokuja kujifunza uzuri .
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment