
Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini Uganda amesema kuwa mkewe na watoto wamelazimika kuikimbia nchi kutokana na ukatili wa vikosi vya usalama katika msako nyumbani kwake.
Robert Kyagulanyi, anayejulikana kama Bobi Wine, alitoa tangazo hilo Jumatano katika ujumbe wa video kwenye mkutano wa kimataifa wa haki za kibinadamu huko Geneva, Uswisi.
Bobi alikuwa mpinzani mkuu wa Museveni katika uchaguzi wa mwezi uliopita, akishika nafasi ya pili kwa asilimia 24 ya kura nyuma ya Rais Museveni aliyepata asilimia 71, lakini tangu matokeo hayo kutangazwa amejificha akisema kuwa vyombo vya usalama vinamsakama ili kumkamata.
Katika ujumbe wake kwenye mkutano wa Geneva, Bobi alitoa wito wa vikwazo dhidi ya Rais Museveni wa Uganda na mwanawe, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kwa ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wapinzani wao.
Alisema bado alikuwa mafichoni katika eneo lisilojulikana si kwa hiari lakini kwa kuhofia kuuawa.
Katika ujumbe uliotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Muhoozi aliandika kwamba “kitu bora kuhusu Bobi Wine ni kwamba sote tumemsahau, na kuongeza kuwa “abaki Geneva milele”.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment