Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaHospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imepokea ugeni wa viongozi wa ngazi ya juu kutoka Shirika la Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) la nchini Marekani. Ugeni huo uliongozwa na Colonel (COL) Brianna Perata, Kamanda wa WRAIR/DOW, akiambatana na maafisa wengine waandamizi, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.Ujumbe huo ulifanya mazungumzo na Uongozi wa Hospitali chini ya Dkt. Godlove Mbwanji, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.Mazungumzo hayo yalilenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nyanja mbalimbali za afya, hususan utafiti, kubadilishana uzoefu, pamoja na maendeleo ya huduma za afya kwa ujumla.Akizungumzia ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani, Dkt. Mbwanji alieleza kuwa hospitali itaendelea kushirikiana na Marekani kupitia programu mbalimbali zilizo chini ya mpango wa PEPFAR, zinazotekelezwa katika mkoa wa Mbeya pamoja na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Rukwa, Katavi na Songwe.Kupitia programu hizo, huduma za afya zimeimarishwa kwa kiasi kikubwa, hasa katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utoaji huduma za afya. Ushirikiano huo unaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya afya katika kanda na taifa kwa ujumla.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment