" IDARA YA AFYA CHUNYA YATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WASIOWAJIBIKA

IDARA YA AFYA CHUNYA YATAKIWA KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WASIOWAJIBIKA

 


Na Lydia Lugakila-Misalaba Media, Chunya – MbeyaMwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mhe. Kelvin Nshinshi, ameielekeza Idara ya Afya wilayani humo kuchukua hatua za haraka kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wananchi kuhusu utendaji wa baadhi ya watumishi wa vituo vya afya.Mhe. Nshinshi ametoa kauli hiyo Februari 4, 2026, wakati akifunga kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitisha bajeti kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.Amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi wakidai kuwa baadhi ya watoa huduma za afya hawatekelezi majukumu yao ipasavyo, ikiwemo madai ya kwenda kazini wakiwa wamelewa pamoja na kutoa kauli zisizofaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma.Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti huyo ameagiza Idara ya Afya kukemea na kudhibiti tabia hizo, akisisitiza kuwa hazikubaliki na zimepitwa na wakati.Ameongeza kuwa kwa sasa kipaumbele kikubwa ni kuwasikiliza wananchi na kuwapatia huduma bora wanapofika katika vituo vya afya ili kujenga imani na kuboresha sekta ya afya wilayani humo.Aidha, Mhe. Kelvin Nshinshi ametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa Halmashauri ya Chunya kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua za maendeleo.“Niwaombe kazi zote mlizopewa na wananchi mzitekeleze kwa uaminifu na weledi, pamoja na kuwasikiliza wananchi kwani kuwajibika ni jambo la lazima,” alisema Mwenyekiti huyo.Hata hivyo, amewahimiza madiwani kufanya kazi kwa usawa, kuwatendea haki wananchi wanaowaongoza na kuhakikisha sauti za wananchi zinasikilizwa na kuheshimiwa wakati wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post