Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Jacob Nkwera, amewataka madiwani katika kata zao kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walioandikishwa kuanza darasa la kwanza wanahudhuria shule kikamilifu.
Nkwera amesisitiza kuwa ni jukumu la pamoja kwa madiwani na watendaji wa kata kuhakikisha watoto wote waliofikisha umri wa kwenda shule wanapelekwa shuleni kwa wakati, hatua itakayosaidia kuepusha changamoto ya watoto kubaki majumbani bila kupata elimu.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na madiwani, watendaji wa kata pamoja na wakuu wa idara mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba, kwa lengo la kuhakikisha changamoto zilizopo katika maeneo husika zinatatuliwa kwa haraka, na hivyo kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Acton Lwankomezi, ametoa shukrani zake za dhati kwa madiwani pamoja na watendaji wote kwa kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuwaletea wananchi maendeleo katika kata zao.
Lwankomezi amesisitiza umuhimu wa madiwani na watendaji kuandaa mipango ya kimkakati na kuiwasilisha Wizara ya Fedha, ili changamoto mbalimbali ziweze kutatuliwa kwa haraka na kwa ufanisi katika maeneo yao.
Vilevile, Mstahiki Meya ameelezea kero ya uwepo wa wanyama aina ya ngedere, ambao wamekuwa changamoto kubwa katika baadhi ya kata za Manispaa ya Bukoba, na kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kulifanyia kazi suala hilo ili changamoto hiyo iweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment