" JESHI LA POLISI MBEYA LAWAFIKIA WENYE UHITAJI

JESHI LA POLISI MBEYA LAWAFIKIA WENYE UHITAJI

 

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya.

Kuelekea maadhimisho ya Siku Maalum ya Familia ya Polisi Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali (OCD), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Salehe Kalulu, amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wilayani humo kutembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Child Hope Tanzania kilichopo Ubaruku.

Katika ziara hiyo, SSP Kalulu amewaongoza askari hao kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo sukari, juisi na pampers kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kuwa na utamaduni wa kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii yenye uhitaji na kuyawezesha kwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali kama sehemu ya kurudisha kwa jamii (Corporate Social Responsibility).




  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post