" POLISI MBEYA WAPANDA ZAIDI YA MITI 100 KUADHIMISHA SIKU YA FAMILIA YA POLISI

POLISI MBEYA WAPANDA ZAIDI YA MITI 100 KUADHIMISHA SIKU YA FAMILIA YA POLISI

MBEYA.

Kuelekea Maadhimisho ya Siku Maalum ya Familia ya Polisi Mkoa wa Mbeya, leo Februari 12, 2026.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, amewaongoza Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali katika zoezi la upandaji miti.

Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mbeya, ambapo zaidi ya miche 100 ya miti imepandwa ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uhifadhi wa mazingira.

Aidha, zoezi la upandaji miti limefanyika katika wilaya zote za Polisi Mkoa wa Mbeya ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya Siku Maalum ya Familia ya Polisi Mkoa wa Mbeya (Police Family Day), yatakayofanyika Februari 14, 2026.







  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post