" KAMANDA MAGOMI AITAKA SUNGUSUNGU SHINYANGA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA JESHI LA POLISI

KAMANDA MAGOMI AITAKA SUNGUSUNGU SHINYANGA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA JESHI LA POLISI

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi maarufu kama Sungusungu kuendelea kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kudumisha ulinzi na usalama mkoani Shinyanga.

Kamanda Magomi ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Lagana, Wilaya ya Kishapu, wakati wa ukaguzi wa vikundi hivyo, ambapo pia aliwahimiza wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kuhakikisha malezi bora na nidhamu kwa wanafunzi kama msingi wa kujenga jamii salama yenye maadili mema.


Post a Comment

Previous Post Next Post